Kichangani Student Centre
Kichangani Student Centre ni kituo maalumu cha vijana kinachotoa fursa mbalimbali za shughuli za kielimu, kijamii, na kisaikolojia. Kituo hiki kinajumuisha:
Ukumbi wa Mgulunde – ukumbi wa mikutano, mafunzo na shughuli za kijamii.
Duka la Vitabu – mahali pa kupata vitabu na vifaa vya kielimu.
Hosteli ya Vijana wa Kiume – makazi salama kwa vijana wanaohudhuria shughuli za kituo.
Kichangani Student Centre kinajitahidi kuwa mazingira salama, yenye motisha na yanayowawezesha vijana kukuza talanta zao, maarifa, na uongozi wa kijamii.
.
