Jumuiya Ya Kolping Tanzania
Utangulizi
Jumuiya ya Kolping Tanzania ni Chama Cha Kitume ndani ya Kanisa Katoliki, kilicho anzishwa na Mwenye Heri hayati Padri Adolph Kolping wa Ujerumani, kwa lengo la kuwaimarisha wakristo wakatoliki kiroho na kimwili katika imani yao.
Padre Adolph Kolping alitangazwa kuwa Mwenye Heri na Baba Mtakatifu Yohana Paulo II tarehe 27/10/1991.
Makao makuu ya Kolping kimataifa yapo jijini Kolon Ujerumani, na katika Tanzania makao makuu ya Kolping yapo Jimbo Katoliki la Bukoba.
Kolping kama chama cha Kitume kinatambuliwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC)
Kolping ilianzishwa nchini Tanzania mwaka 1989 na hayati Monsinyori David Kamugisha, wa Jimbo Katoliki la Bukoba, baada ya kutembelea ujerumani na kukuta chama hiki cha Kitume kikifanya kazi nzuri ya kiroho na kimwili.
Kwa sasa Kolping inafanya kazi katika majimbo Katoliki 20 nchini Tanzania, abayo yamegawanyika katika kanda tano ambazo ni:
- Kanda ya Ziwa (Mwanza, Musoma, Bunda, Geita, Bukoba, Ruenge-Ngara na Kayanga
- Kanda ya Kati (Dodoma, Singida na Mbulu)
- Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam, Arusha, Morogoro, Tanga na Same)
- Kanda ya Magharibi (Tabora, Kigoma na Sumbawanga)
- Kanda ya Kusini (Songea na Iringa)
Kolping Tanzania ina mpango wa kueneza utume wake katika majimbo Katoliki yote nchini Tanzania.
Malengo Ya Kolping Kiroho Na Kimwili
- Kulinda na kuheshimu Hadhi na Utu wa mtu kwa mawazo, maneno na matendo.
- Kumsaidia mtu aweze kuziendeleza nguvu zake, karama na vipaji alivyojaliwa na Mwenyezi Mungu kwa njia ya Ubatizo.
- Kuwafanya wanachama wake waishi maisha ya Sala kwa kushiriki Ibada na Sakramenti kupitia walezi kwa kiroho mapadri na walimu wa dini makatekista.
- kuongeza ujuzi wa wanachama katika nyanja mbali mbali za maisha na kufanya kazi kwa bidii (SALA, ELIMU na KAZI) kwa kuwapa semina na uwezeshwaji pale inapowekekana, ili walitegemeze Kanisa kwa sadaka na matoleo yao na pia kuimarisha familia na kayaz ao.
Kolping Kanda Ya Kusini
Kolping Kanda ya kusini (Iringa na Songea) ilianza kazi zake mwaka 2015. Ofisi za Kolping Kanda ya Kusini zipo Kanisa Kuu la Jimbo la Iringa Parokiani Kihesa, kwenye Jengo la Maendeleo.
Mpaka sasa Kolping Kanda ya Kusini inafanya utume wake katika Parokia 8 Jimbo kuu la Songea na Parokia 7 Jimbo la Iringa.
Parokia hizo kwa Songea ni Lizaboni, Ruhuwiko, Nakahuga, Mgazini, Lusonga, Magagura, Mpitimbi na Kitanda.
Kwa jimbo la Iringa Kolping ipo katika Parokia za Ifunda, Lyasa, Mgama, Kaning’ombe, Ismani, Kilolo na Madege.
Kuna mpango wa kuongeza familia za Kolping katika Parokia zote za Jimbo Kuu la Songea na Jimbo la Iringa; pia Kupanua utume wa Kolping kwenye majimbo yote Katoliki nchini Tanzanai.
Shughuli za Kolping katika kanda ya Kusini
- Semin a za kilimo bora
- Ufugaji bora wa nguruwe na mbuzi
- Utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti ya matunda, mbao, malisho, kuhifadhi vyanzo vya maji, nk.
- Kuwezesha mshine za kupukuchua mahindi
- Kuwezesha pumpu za kilimo cha umwagiliaji
- Kutoa mbegu bora za mahindi na mbogamboga
- Mifumo ya kuweka na kukopa (HISA/SACCOs)
- Kuhifadhi mzao vizuri kwenye vihenge vya kisasa na mifuko ya PICS
Mafanikio
- Kuongezeka kwa mavuno hasa mahidi kutoka gunia 3 kwa ekari hadi gunia 15 kwa ekari
- Lishe bora ngazi ya kaya
- Kuongezeka kwa kipato ngazi ya kaya kwa kuuza mazao yatokayo shambani na mifugo.
- Kongezeka kwa matoleo Kanisani (Fungu la 10)
- Ongezeko la kubariki sakramenti ya ndo kwa wana Kolping.
- Kutegemeza Kanisa kwa majitoleo ya hali na mali.
Picha Mbalimbali
