Call Us:+255 752 84 02 70
HISTORIA FUPI
Eneo la Nyabula kama Parokia lilikuwa ni eneo lote la Udzungwa yakiwemo maeneo ambayo baadaye yalitengwa na kufanywa parokia. Maeneo hayo ni Kilolo, Usokami, Ng’ingula na Madege. Hata hivyo eneo letu bado ni kubwa na lina vigango 23 ambavyo vimegawanyika katika kanda tatu:
Kanda ya Nyabula: Nyabula, Ikuvilo, Kitayawa, Tagamenda, Wangama, Igula, Mlanda, Malulumo.
Kanda ya Ihimbo: Ihimbo, Ndiwili, Itimbo, Lukago, Utengule, Isoliwaya, Iwindi, na Italula.
Kanda ya Magulilwa: Magulilwa, Negabihi, Msuluti, Kinyaminyi, Ng’enza, Lupembelwasenga na Itwaga.
Tangu Parokia ianzishwe miaka 89 iliyopita kuna wakatoliki zaidi ya 30,000 ndanimo wakiwemo watawa wa kike 34, watawa wa kiume 7, Mapadre Philipo Mihafu (Marehemu), Beatus Mhaluka, Askofu Paskali Kikoti – Mpanda (sasa Marehemu), Cyprian Mvanda IMC na Isaya Tovagonze na Fr. Simon Luhwago.
Br. David Nyamba – SCIM.
.
Mtumikieni Bwana kwa furaha; Njooni mbele zake kwa kuimba. Zaburi 100:2.