Pd. Martin Mhavile - Paroko

CHOSI
S.L.P 2 CHIMALA – Ilianza 1960
Msimamizi wa Parokia ni Mtakatifu Pius X.
Sikukuu ni 21/08
Umbali toka Makao Makuu ya Jimbo ni Km 257.
+255

CHIMBUKO LA JINA CHOSI

Jina Chosi linatokana na neon la kisangu SHOONSI. Likimaanaisha kuchimbuka kwenda chini na kupanuka kwa pembeni. Shoonsi inaonekana ulikuwa ni mfereji ambao ulichimbwa na mzungu mwanamke Mjerumani aliyejulikana kwa jina la SIMBEYANJE.

Hivyo basi jina la Chosi asili yake ni Mto Chosi Unaopatikana maeneo ya Masasi, kwani eneo la masasi ndiko kulikuwa kituo cha makatekista kutoka Ujewa kufundisha Wakatekumeeni na dini kwa ujumla. Makatekista hao ambao siku hizo walijulikana kama walimu wa dini n; Rodrick, Filipo Makuku, Andreas, Yeremiasi Mwilongo.

Kazi ya kuhubiri dini katika maeneo ya Masasi ilifanikiwa kwa kiwango kikubwa, kutokana na ruhusa ya chifu Merere, ambaye alimtuma mwanae mkubwa, aliyeitwa Malangalila Ga – Moto Khahemele kuongoza maeneo ya Chosi kama makao makuu ya chifu Malangalila. Chosi iliendelea kuwa sehemu ya kigango cha Ujewa kwa Muda wa takribani miaka 20, yaani kutoka mwaka 1940 -1960.

Sermons

Kuanzishwa kwa Parokia ya Chosi

Mnamo mwaka 1960 baada ya waamini kuongezeka Pd Emilio Chiuch alianzisha Parokia ya Chosi katika eneo la Mwakadama. Mwakadama lilikuwa ni jina la mtu, yaani mkazi wa eneo hili Ternea alikuwa (Mnjajila wa Mtwa Malangalila) Jumbe wa Chifu ambayee alitoa eneo kwa wamisionari kwa kujenga shule na kanisa, ndipo Padri Chiuch akaanza kujenga shule na kanisa mwaka 1960.

Mapadri Waliohudumia Parokia ya Chosi Toka 1960 -2021

Pd Emilio Chiuch 1960 – 1965, Pd Dino Baretta 1965 – 1966, Pd Truch 1966 – 1969, Pd Mario Arte 1969 – 1978, Pd Ante Batarelo na Pd Bosko 1978 – 1981, Pd Stipe 1981, Pd Giovan Giorda 1981 – 1988, Pd Angello Pizzaia 1988 – 1994, Pd Francis Mdemu 1994 – 1996, Pd Virgilio Panero 1995 – 1997, Pd Dino Baretta 1996 – 1997, Peter Lumiri 1998 – 1999, Pd James King’ori 1998 – 1999, Leopold Mlimbo 1999 – 2010, Pd Leonard Maliva 2004 – 2006, Pd Alex Mkalawa 2006 -2010, Pd Sostenes KIbiki 2010-2015, Pd. Martin Mhavile 2006 hadi sasa

Wakristo Waanzilishi wa Parokia

Wakristo waannzilishi wa Parokia ya Chosi ni Thomasi Mwalusawulwa Mwidunda, Rustika Mjane wa Katekista Yeremiasi Mwilongo, William Yereasi Mwilongo, Augustino Sanga na Mkewe aliyesaidia ujenzi wa Kanisa kama mpishi.

Vigango

Parokia ina vigango vifuatavyo, Chimala, Chosi, Ukwavila, Mbuyuni, Mabadaga, Itamba, Utulo, Siteone, Msesule, Majombe, Mapogoro, Kibaoni, Ruaha na Kimani.

Vitongoji.

Ifushilo, Mngolongolo, Chang’ombe na Mlangali.

.

Masista Wazawa.

Masista wazawa wa Parokia ya Chosi ni Sr. Leokadia Mkwame, Sr. Stella Patrick Kamwela, Sr. Teodosia Mbwiga, Sr. Jema Chaula, Sr. Eugemia Lubida na Sr. Concepta Kozimbili.

forging A Relationship with God.

DateJune 21

Time: 4:00 pm – 8:00 pm

Senectus erat sem tincidunt mi duis vehicula, est diam molestie. Mauris in ut eget wisi, et mollis bibendum nulla, amet malesuada.

Mount Vernon Annual Youth Retreat

DateJune 26-29

Meet: 7:00am Church lot

Senectus erat sem tincidunt mi duis vehicula, est diam molestie. Mauris in ut eget wisi, et mollis bibendum nulla, amet malesuada.

Et ligula sit quam, sapien lorem. Nec risus lorem vestibulum mi facilisis. Tincidunt urna accumsan nec, risus fermentum.

Senectus erat sem tincidunt mi duis vehicula, est diam molestie.
Mauris in ut eget wisi, et mollis bibendum nulla, amet malesuada.