Ofisi ya Afisa Tawala – Jimbo la Iringa

Ofisi ya Afisa Tawala wa Jimbo la Iringa ina jukumu la kusimamia masuala ya kiutawala, uratibu wa shughuli za ofisi za jimbo, pamoja na kuhakikisha utekelezaji mzuri wa maamuzi na sera za Jimbo kwa kushirikiana na parokia, taasisi na idara mbalimbali.

Afisa Tawala husaidia Askofu wa Jimbo katika kusimamia rasilimali watu, mali na shughuli za kila siku za kiutawala, huku akihakikisha uwajibikaji, ufanisi na uadilifu katika utoaji wa huduma. Ofisi hii pia ni kiungo muhimu kati ya uongozi wa Jimbo, taasisi zake, na wadau mbalimbali wa maendeleo.

.