Huduma ya Hostel – Booking & Reservation

Jimbo Katoliki la Iringa linakaribisha wageni wote kutumia huduma zake za Hostel, zinazotoa malazi salama, tulivu na yenye heshima kwa muda mfupi au wa kati. Hostel zetu zinafaa kwa wanafunzi, wahudumu wa kanisa, wageni wa taasisi, washiriki wa semina na makongamano, pamoja na wageni binafsi.

Sifa za Hostel

  • Vyumba safi na salama

  • Mazingira tulivu na yenye heshima

  • Maji safi na umeme wa uhakika

  • Usalama wa kutosha

  • Mahali panapofaa kwa kupumzika na kujisomea

Jinsi ya Kufanya Booking / Reservation

Ili kufanya booking ya malazi:

  • Wasiliana nasi kupitia simu: 0767873842, 0765750303 &  0769064523 au barua pepe: dioceseofir@hotmail.com

Timu yetu itakuthibitishia upatikanaji wa chumba na kukupa maelezo zaidi kuhusu gharama na taratibu za malipo.

Karibu Ukaribishwe

Tunakaribisha wageni wote kufurahia huduma ya malazi katika mazingira ya amani, utulivu na maadili mema.

Kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu

Kanisa kuu la dayosisi hiyo lipo Iringa kilomita chache kutoka katikati ya jiji eneo la Kihesa.