Zaidi ya watoto 700 wabatizwa Parokia ya Kihesa

Zaidi ya watoto 700 kutoka katika vigango saba (7) vya Parokia ya Kihesa Jimbo Katoliki la Iringa wamepatiwa sakramenti ya nubatizo kwenye Kanisa Kuu la Moyo Mt. wa Yesu Parokia ya Kihesa.

Misa hiyo ya ubatizwa imeadhimishwa kwenye viwanja vya parokia hiyo Dominika ya Sikukuu ya Moyo Mtakatifu wa Yesu ambaye ni msimamizi wa Jimbo la Iringa na Parokia hiyo,na kuhudhuriwa na maelefu ya waamini kutoka ndani na nje ya parokia hiyo.

Mapadre walioungana na Paroko wa Kihesa katika kutoa sakaramenti ya ubatizo ni pamoja na paroko Msaidizi wa Parokia hiyo Padre Steven Msigwa, Padre Fidelis Mgimwa, Padre Beda Kiure, Padre Isdory  Qaya na Padre Venance Ndalichako


Awali kabla ya kuanza kwa Misa Takatifu, Paroko wa Parokia hiyo Padre Steven Mvili, amesema kuwa idadi hiyo kubwa ya wabatizwa ipo kwenye makundi tofauti.

Kundi mojawapo Padre Mvili amesema ni kundi la wazazi ambao wameishi kwenye uchumba sugu na wameamua kufunga ndoa na kurudi kwenye masakramenti ” leo hii tunashuhudia kundi hili kubwa la wabatizwa, baadhi ya wazazi wa watoto hao wameamua kuachana na uchumba sugu, na ndiyo maana kwenye matangazo yetu ya ndoa kuna ndoa zaidi ya 60 zitafungwa hivi karibuni, tumeona nia yao njema na ndiyo maana watato wao tumewabatiza leo” amesema Padre Mvili na kuongeza kuwa


“Kundi jingine utakumta mzazi mmoja awe wa mwanaume au mwanamke na ameamua kurudi kwenye masakramenti nao pia watabatizwa, lakini kundi jingine ni wale watotot ambao wanaishi na bibi na babu yani hawana wazazi kutokana na sababu mbalimbali”

Pamoja na ubatizo huo Paroko huyo pia ametoa sakaramenti ya kipaimara kwa watu wazima wapatao 2.Akitoa homilia kwenye misa hiyo Padre Fidelis Mgimwa ambaye ni mhadhiri wa chuo Kikuu cha Kikatoliki Ruaha (RUCU) amesema wanafuraha siku hiyo kwa sababu wapo pampoja na wale wenye uchumba sugu ambao wameamua kurudi kwenye

masakramenti na wanabatiza watoto ni neema ya Mungu amabyo imewasukuma hapo na iwasukume hadi watakapofikia hatua ya kufunga ndoa. Akitolea mfano wa Nabii Hosea, Padre Mgimwa amesema kwamba alimvumilia mkewe pamoja na kwamba alikuwa ni mkorofi.

“Nabii Hosea  alikuwa na bahati mbayaq, katika unabii wake na kazi yake alioa mwanamke asiemtulivu lakini alimvumilia tu, wala hakumuacha pamoja kwamba alizaa watoto watatu..huyo ndiye mke wa Nabii, katika hilo Mungu hakumuambia hufai kuwa Nabii, ndivyo hata anapowakumbatia wenye dhambi wala hawaachi” amesema Padre Mgimwa.

Aidha Padre Mgimwa amewapongeza wanashirika la Moyo  Mtakatifu wa Yesu ambao ki parokia hufika kanisani kila  alhamisi kusali, wanawaombea,wanaiombea na parokia yao na ulimwengu wote, na kila Ijumaa ya kwanza ya mwezi wanakesha kanisani, amesema Padre Mgimwa kwamba ” hawa ni marafiki wa Yesu,Mungu awafunulie hekima na awajalie neema kuyatangaza mema yote Ulimwenguni”mwisho