Education Office
Kanisa katoliki linatambua kwamba kila binadamu ana haki ya msingi ya kupata elimu makini bila kujali itikadi za kisiasa, kidini, kijinsia, kabila au taifa.
Education Cordinator
Jimbo la Iringa lina jumla ya taasisi 61 za elimu ikiwa shule za awali ni 22 Msing ni 9, sekondari ni 18, seminari 3, vyuo vya ufundi ni 8, na chuo cha kilimo na mifugo 1.
Utangulizi
Ni ukweli usiopingika kuwa kanisa Katoliki Tanzania limekuwa kati ya wadau wakubwa wa maendeleo katika sekta ya elimu kabla na baada ya uhuru katika taifa letu. Mchango wa kanisa Katoliki katika utoaji wa huduma ya elimu umekuwa kuanzia shule za chekechea, awali, msingi, sekondari, vyuo vya ufundi stadi hadi elimu ya juu.
Kanisa katoliki linatambua kwamba kila binadamu anahaki ya msingi ya kupata eelimu makini bila kujali itikadi za kisiasa, kidini, kijinsia, kabila au taifa. Lengo kuu la elimu Katoliki ni kumfunda mtu mzima; kiakili, kimwili, kiroho, kijamii na kimaadili, kwa kufanya hivyo, shule za kikatoliki zinawaanda vijana wa kike na kiume kwa kesho iliyo bora zaidi.