Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa Jubilei Miaka 50 ya Daraja Takatifu ya Upadre
Askofu Tarcisius J.M. Ngalalekumtwa anawaalika Mapadre kumtazama na kumtafakari Kristo Yesu aliyejitoa kama: Mwalimu, Mchungaji na Kiongozi, akaonesha uaminifu, utii na upendo usiokuwa na mipaka kwa waja wake. Uaminifu wa Kristo uwe ni changamoto ya uaminifu wa Mapadre unaojionesha kwa namna ya pekee katika: upendo, unyofu, unyenyekevu, huruma na huduma makini kwa watu wa Mungu….