Mhashamu Baba Askofu Ngalalekumtwa azindua miaka 50 ya WAWATA Jimbo

Mhashamu Askofu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa akiwa ameshika mshumaa wa Yubilei ya miaka 50 Wawata Kijimbo ikiashilia uzinduzi wa Yubilei hiyo.

MHASHAMU Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa amezindua Yubilei ya Miaka 50 ya Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) kwa Jimbo la yaliyoadhimishwa kwenye Kanisa Kuu la Kiaskofu la Moyo Mtakatifu wa Yesu Parokia ya Kihesa.

Mwenyekekiti wa WAWATA taifa, Bi. Evelin Malisa Mtenga amesema kwamba amesewataka akina mama hao watambue kwamba wao ni jeshi kubwa na kazi wanayoifanya kwa uchache wao lakini inaonekana ni kubwa.

Baadhi ya WAWATA Jimbo la Iringa kutoka Parokia mbalimbali wakiwasha mishumaa kutoka kwenye mshumaa ambao umewashwa na Mhashamu Baba Askofu Ngalalekumtwa kwenye uzinduzi wa miaka 50 ya WAWATA Kijimbo.

Amesema kwamba kila wanachokifanya wahakikishe wanafanya kwa nia ya kuendeleza utume wa mwanamke mkatoliki na zaidi kazi za utumishi wa kanisa.

“Sisi kama wana wake wakatoliki wanakumbushwa walipobatizwa walipewa ahadi ya kuwa makuhani waliewa hadhi ya kuwa wafalme na manabii, kazi pia kumtangaza Yesu mfufuka sio kuwaachia maklero wala mababa wa kiroho.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo inasema “Miaka 50 ya WAWATA Upendo Mshikamano na Uadilifu wa Uumbaji”

Mgeni rasmi kwenye sherehe hizo alikuwa ni mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Queen Curthbet Sendiga ambaye ameahidi kushirikiana na akina mama hao kwa pamoja na akawakumbusha umuhimu wao katika kulea familia.

Takribani parokia ziapazo 24 kati ya 44 za Jimbo wamehudhuria uzinduzi wa Yubilei hizo ambapo pia Mhashamu Askofu aliwasha mshumaa kama alama ya uzinduzi huo.

Similar Posts

3 Comments

  1. Very nice post. I simply stumbled upon your blog and wanted to mention that I’ve truly enjoyed surfing around your blog posts. In any case I will be subscribing on your rss feed and I am hoping you write again soon!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *