Kigango cha Mgama sasa ni Parokia rasmi

Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa Mhasham Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa katika picha na Paroko wa kwanza Parokia ya Mgama Padre Augen Ngatunga (Kulia kwa Askofu) kushoto kwa Askofu ni Padre Vincent Mwagala Makamu wa Askofu Jimbo la Iringa pia ni Paroko wa Parokia ya Ifunda.

Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wa Jimbo Katoliki la Iringa hivi karibuni amezindua Parokia mpya ya Mgama na kumteua Padre Augen Ngatunga kuwa paroko wa kwanza wa parokia hiyo.

Hapo awali Parokia hiyo ilikuwa ni kigango cha parokia ya Ifunda.

Pamoja na kuzindua parokia hiyo ambayo inalifanya Jimbo kuwa na idadi ya parokia 44, pia askofu Ngalalekumtwa ametoa sakramenti ya kipaimara kwa watoto wapatao 305 kutoka parokia ya Mgama na Ifunda.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *