Ibada ya Maadhimisho ya Upadrisho 25-26 Agosti 2021
Tunafurahi kwamba Mwenyezi Mungu amewachagua hawa makuhani kutoka katika familia ya wabatizwa wa Jimbo la Iringa; ili awaweke wakfu kwa ajili ya mambo matakatifu yamhusuyo Mungu katika mpango wake wa kuwakomboa wanadamu.
Maana kila kuhani mkuu aliyeteuliwa katika wanadamu amewekwa kwa ajili ya wanadamu katika mambo yamhusuyo Mungu; ili atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi (Ebr. 5:1)
Wapendwa katika Kristo, niwaalike nyote kuwaombea mapadre wwapya; ili waishi kitakatifu wakijibidiisha kufananisha mioyo yao na Moyo Mtakatifu wa Yesu uliojaa mapendo na huruma. Mioyo yao ikifanana na Moyo Mtakatifu wa Yesu, kwa hakika itawavutia watu wengi kwa Mungu. Mwenyezi Mungu awajalie ukarimu wa kiuchungaji;
“Ili waweze kulihudumia kundi kwaa jirani hivi, kiasi cha kunukia harufu ya kondoo”, kama anavyofundisha Baba Mtakatifu Fransisko. (Katika Homilia yake Siku ya Adhimisho la Misa ya Krisma, Kanisa la Mt. Petro, mjini Vatikan, tarehe 28.03,2013)