|

Adhimisho La Kilele Cha Yubilei Ya Miaka 125 Ya Uinjilishaji Iringa Na Miaka 50 Ya Upadre Wa Askofu Tarcisius J.M. Ngalalekumtwa

Walioongoza Jimbo la Iringa

Historia Ya Baba Askofu Mhashamu Tarcisius J.M Ngalalekumtwa

Askofu Tarcisius J.M Ngalalekumtwa alizalkiwa tarehe 25.10.1948 katika kijiji cha Banawanu kilichopo Parokiani Tosamaganga. Wazazi wake ni Joseph Ngalalekumtwa na Mama ni Magdalena Sekutika. Alibatizwa Parokiani Tosamaganga tarehe 15.11.1956. na siku hiyo alipewa Sakramenti ya Kipaimara na Mhasahamu Askofu Attilio Betramino, I.M.C na Komunyo ya Kwanza.

Kanisa la Tosamaganga

Mwaka 1956 alianza masomo ya Elimu ya msingi katika shule ya msingi ya wavulana ya Tosamaganga ambayo sasa inaitwa shule ya msingi Lupalama A. aliendelea na masomo katika shule hiyo hadi mwaka 1959., Mwaka uliofuata alijiunga na seminari ndogo ya Tosamaganga ambapo alisoma hadi mwaka 1967. Akiwaka na mwito wa kumtumikia Mungu katika upadree, aliamua kuendelea na masomo ya seminarini. Hivyo mwaka 1968 alipelekwa Peramiho kujiunga na seminari kuu kwa masomo ya Falsafa. Mwaka 1969 alitumwa Roma, Italia kusomea Teolojia katika Chuo Kikuu cha Propaganda Fide. Alisoma Chuoni hapo hadi mwaka 1974 ndipo alipohitimu vizuri masomo yake na kujipatia Stashahada katika fani hiyo ya Elimu ya Mungu sadikifu (Licence in Dogmatics.) tarehe 07.04.1973 alipata Daraja Takatifu ya Upadre huko San Ginesio, Camerino, Italia. Daraja hiyo alipewa na Mhashamu Askofu Bruno Frattegiani

Akiwa Padre tayari alirudi Tanzania Oktoba 1974. Mhashamu Askofu Mario A. Mgulunde alimtuma Padre Tarcisius J.M Ngalalekumtwa Parokiani Ifunda. Huko alifanya kazi kuanzia 18.11.1974 hadi 05.12.1976. Anakumbukwa na wana Parokia ya Ifunda kama mchapakazi sana, asiyependa makuu. Alikuwa tayari kusikiliza shida za watu bila kuchoka.

Parokia ambayo aliikuta ikiwa nyuma kimaendeleo na kidini, alichangamsha sana. Aliiwezesha Parokia hiyo kufikia kiwango kikubwa katika shughuli za kujitegemea kiuchumi. Alikuwa Mchungaji mahiri katika Nyanja mbalimbali. Utaratibu na Ukarimu wake uliwavuta vijana wengi wa kike kujiunga na Utawa, na hali kadhalika Miito ya Kipadre ilistawi sana Parokiani hapo, kwani vijana wengi walipata Wito wa kujiunga seminarini kwa nia ya kutaka kuwa Mapadre.

Kutokana na bidii zake nyingi alizoonyesha Padre Tarcisius J.M. Ngalalekumtwa, kwa matendo na mifano mizuri, Askofu Mario A. Mgulunde alimpeleka Seminari Kuu ya Peramiho kama mkufunzi. Naye alikubali kwa furaha kwenda huko Peramiho mwaka 1977. Na haukupita mda mrefu aliteuliwa kuwa Gombera wa Seminari hiyo kushika nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na mtangulizi wake Padre

Tangu kuingia kwake Iringa kama Askofu wa Jimbo hilo, Parokia zimeongezeka, mpaka sasa jimbo lina jumla ya parokia 45 (attache link)

Masuala ya afya hayakuachwa nyuma. Zahanati zimeboreshwa na hata kujenga nyumba za wahudumu wa afya, Kilolo ikiwa ni kielelezo. Chuo cha Uuguzi na Ukunga cha Tosamaganga kimefunguliwa ili kuboresha huduma za afya. Hali kadhalika suala la Elimu limekuwa ni jambo lenye umuhimu wa pekee kati ya shughuli zake. Kituo cha malezi ya Watoto Wadogo Malangali kimejengwa wakati wake japo wazo lilikuwepo wakati wa mtangulizi wake.

Kwa kuwa Mhashamu Askofu Tarcisius J.M Ngalalekumtwa bado analihudumia jimbo hili, itakuwa ni mapema mno kusema mambo yaliyofanywa naye. Kuna mambo mengi ambayo anayafanya, na hasa katika masuala ya Elimu, Afya pamoja na mambo ya kiuchungaji kwa ujumla. Aidha kama Askofu ameshirikiana na maaskofu wenzake katika Baraza lao, hata akalisimamia kama Raisi wa baraza hilo kwa miaka kadhaa; kabla ya Askofu mkuu Gervas Nyaisonga, aliepokea cheo hicho baada yake. Tunapompongeza kwa kazi hiyo njema. Tunawashukuru Maaskofu wote kwa ushirikiano wao mwema kwake. Aliwahi kuliongoza jimbo la songea kama Askofu msimamizi wa jimbo hilo baada ya Askofu Norbert Mtega kustaafu. Tunampongeza kwa kazi nyingi alizofanya tunamwombea afya njema na utume mwema.

Unaweza kufwatilia Matangazo yetu kwenye YouTube Channel yetu, ya Jimbo la Iringa hapa chini, Usisahau KU Subscribe, Like na Kushare kwa marafiki.

Similar Posts